News

Wahudumu wa boda boda Mariakani-Kilifi walalamikia utovu wa usalama.

Published

on

Wahudumu wa boda boda huko Mariakani eneo bunge la Kaloleni kaunti ya Kilifi wanatilia shaka ongezeko la watu wanaojifanya wanabodaboda ilihali watekeleza visa vya uhalifu eneo hilo.

Mwenyekiti wa wahudumu hao Gitome Mwasia alisema kwa sasa wameanza mchakato wa kuwasajili wahudumu wote wa bodaboda katika kila kituo eneo hilo.

Mwasia aliongeza kuwa hatua hiyo itarahisisha wao kuwatambua wahudumu halali wa eneo hilo.

Wakati huo huo mwenyekiti huyo alisisitiza haja ya kila mwanabodaboda eneo hilo kujisajili akisema hatua hiyo itawasaidia kutambua wahalifu wanaotumia kigezo cha wanabodaboda kutekeleza visa vya ujambazi.

Vile vile aliwashauri wahudumu hao kuwa makini wanapobeba abiria huku akiwashinikiza wakazi wa eneo hilo kutowaficha wahalifu bali watoe habari muhimu kwa vitengo husika.

Taarifa ya mwanahabari wetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version