Business
Wafugaji wa Nyuki wanaitaka serikali kuwawezesha kibiashara
Wafugaji wa Nyuki eneo la Mida kaunti ya Kilifi wameitaka serikali kuu na zile za kaunti kukumbatia Kilimo cha Nyuki ili kuendeleza uzalishaji wa Asali na kuchangia mapato zaidi kwa jamii.
Kulingana na wafugaji hao, serikali hazijakumbatia ufugaji wa Nyuki jambo ambalo walisema limesababisha mapato duni kwa wakulima.
Wakizungumza na CocoFm, wafugaji hao walisema Kilimo kama vile Mahindi, Matunda na hata misitu inategemea Nyuki ili kuzalisha mazao kwa wingi hivyo kukumbatia ufugaji wa Nyuki ni kukumbatia mazao bora.

Wakulima wa ufugaji nyuki wakiendeleza kilimo{picha kwa hisani}
Wakati huo huo waliitaka serikali kuwawezesha wafugaji wa Nyuki humu nchini ili kuendeleza biashara zao bila changamoto zozote.
”Nyuki ndio wajenzi wakubwa wa msitu na kilimo kama vile cha Mahindi na Matunda na bora kwani huimarisha mazao na serikali inapaswa kuwasaidia wafugaji na kuwawezesha ili kuimarisha uvugaji wa nyuki na kuboresha mazao”, walisema wakulima.
Taarifa ya Pauline Mwango