Business
Wafanyibiashara waonya waandamanaji kutoharibu mali ya umma
Wafanyibiashara mjini Kilifi kaunti ya Kilifi wamewataka vijana kuwa makini wakati wa maandamano ili kuepuka uharibifu wa mali.
Kulingana na wafanyibiashara hao kumekuwa na uharibifu wa mali huku wengi wakikadiria hasara kila wakati vijana wanapoandama nchini
Wakizungumza na Coco Fm, wafanyibiashara hao walisema maandamano ya mwaka jana yaliwasababishia hasara kwani waandamanaji waliharibu mali ya umma.
“Mwaka uliopita wakati wa maandamano ya Juni 25, kulipata hasara nyingi na hakuna fadia tulipewa na serikali, sasa sisi hatujakataa maandamano ni haki ya wakenya kuandamana lakini tafadhali wasiharibu biashara zetu, tunatafutia watoto wetu kwa sababu maisha ni ngumu Kenya”, walisema wafanyibiashara hao.
Aidha walisema endapo taifa hili litashuhudia maandamano ya mara kwa mara basi huenda sekta ya biashara nchini ikazorota kwa kiwango kikubwa.