County
MCK Yawataka Wanahabari Kuzingatia Maadili ya Taaluma Yao
Baraza la vyombo vya habari nchini MCK limewataka Wanahabari kuzingatia maadili ya taaluma yao wakati wa kuripoti taarifa mbalimbali nchini ikiwemo maswala la uchumi wa bahari.
Mshirikishi wa Baraza hilo kanda ya Pwani Maureen Mudi amesema Wanahabari wanastahili kufahamu kwa kina masuala ya uchumi wa bahari kwani wengi wao wamekuwa wakizamia maswala ya kisiasa.
Kulingana na Maureen, ni aibu kwa Wanahabari kuripoti habari za uongo hasa kwa masuala muhimu yanayoihusu nchi, akisema hali hiyo inashusha hadhi ya vyombo vya habari nchini.
Wakati uo huo amedokeza kwamba Baraza la vyombo vya habari nchini MCK linawashirikisha Wanahabari katika mafunzo ya kila mara ili kuwawezesha kufahamu zaidi masuala ibuka na jinsi wanavyopaswa kuripoti matukio mbalimbali nchini.