News

Rais Ruto atetea rekodi ya utendakazi wa serikali.

Published

on

Rais William Ruto amesema kuwa atahakikisha miradi ya maendeleo aliyoahidi inakamilika kabla ya muhula wake wa kwanza kukamilika.

Rais akizungumza baada ya kikao cha baraza la mawaziri alichambua kwa mapana ahadi za serikali yake zilipofikia.

Rais alishikilia kuwa hana haja ya kuchaguliwa kwa muhula wa pili kwa sasa, ila kufikia mambo aliyoyaahidi yaafikiwe kwa wananchi.

Kiongozi wa taifa aliosoa wanaopinga sera zake akisema lengo lake ni kukamilisha ahadi zake katika muhula wa kwanza na wala sio wapili.

Mkutano huo ni watatu kwa mawaziri na viongozi serikalini kufanyika chini ya uongozi wa rais William Ruto.

Rais vile vile alihimiza mawaziri kuwajibikia sekta muhimu kama vile kilimo, afya, biashara ndogo, teknolojia, nyumba na ubunifu wa uchumi kutoka kwenye mtandao  na elimu.

Taarifa ya Joseph Jira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version