News

Rais Ruto aonya maandamano ya vurugu nchini

Published

on

Siasa za majibizino kuhusu mtizamo wa vijana wa kizazi cha Gen Z na mabadiliko ya kiuongozi nchini zimeanza kushamiri huku rais William Ruto akionekana kuchukizwa na jinsi taifa lilivyosheheni maandamano ya kila mara.

Akizungumza katika eneo la Kilimani jijini Nairobi, Rais Ruto alisema viongozi wa wahuni nchini wataandamwa na mkono wa sheria, akisema wahuni wanaopora mali ya umma na zile za watu binafsi ni lazima wakome.

Rais Ruto alisema hatakubali kuona taifa likishuhudia maandamano ya vurugu na ghasia, siasa za uchochezi, kuchama biashara za wananchi, kuharibu mali ya umma, akisema watu kama hao ambao ni wahuni wanafaa kukabiliwa kikamilifu bila huruma.

Kiongozi wa nchi, hata hivyo aliahidi kulinda mali ya umma, usalama wa wananchi, kutetea na kulinda Katiba ya Kenya, akisema ni jukumu la serikali kuhakikisha inakomesha maandamano ya vurugu na uharibufu wa mali ya umma.

Mda mfupi baadaye, aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua ambaye pia ni Kinara wa Chama cha DCP, alijitokeza na kudai kwamba hakuna jamii inayolenga kuindua serikali huku akiwataka vijana wa Gen Z kujisajili kama wapiga kura ili kumbandua mamlakani rais Ruto wakati wa uchaguzi mkuu.

Taarifa ya Elizabeth Mwende

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version