IEBC: Uchaguzi wa Ol Kalou utakuwa huru na haki

IEBC: Uchaguzi wa Ol Kalou utakuwa huru na haki

Baada ya kushuhudiwa kampeni za vurugu, hongo na uchochezi dhidi ya wananchi wa eneo bunge la Ol Kalou kaunti ya Nyandurua kabla ya uchaguzi mdogo, sasa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC inasema imejipanga vyema kuandaa uchaguzi huo mdogo wa eneo bunge hilo.

Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon, alijitokeza kwa kishindo na kuanza kwa kutoa onyo kali kwa wagombea wote wanaomezea mate kiti hicho.

Katika kikao na Wanabahari, Ethekon alisema IEBC inachukulia kwa uzito sajili ya wapiga kura, na akawaonya wananshi dhidi ya kuwachochea wananchi kufisha vitambulisho vyao, akisema tabia hiyo haitakubalika.

“Tunachukulia kwa uzito sana sajali ya wapiga kura ya Ol Kalou na tunatoa onyo kali kwa wagombea wote wanaomezea mate kiti hicho kuzingatia sheria na kwmaba tutaruhusu ajenti mmoja pekee katika kituo cha kupigia kura na hakuna mtu anaruhusiwa kupiga picha”, alisema Ethekon.

Kwa upande wake Inspekta Jenerali wa polisi nchini Douglas Kanja aliwaonya vijana dhidi ya kushawishiwa vibaya na kuvuruga zoezi la uchaguzi huo mdogo, akisema tayari zaidi ya maafisa wa polisi elfu moja wametumwa Ol Kalou kushika doria.

“Tuko na maafisa wa zaidi ya elfu moja tumewatuma Ol Kalou kushika doria na tunawaonya vijana dhidi ya kushawishi vibaya na kuvurugu zoezi la uchaguzi huo, hiyo hatutakubali. Tunataka uchaguzi uwe wa amani”, alisema Kanja.

Mwenyekiti wa Tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC Kepha Omae amewataka wanasiasa kukoma kuwachochea wananchi na kukumbatia amani, akisema Kenya inahitaji utulivu kuliko siasa za chuki.

Uchaguzi huo mdogo wa eneo bunge la Ol Kalou umeratibiwa kufanyika Julia 16 siku ya Alhamis huku zaidi ya wapiga kura elfu 72 wakiwa wamesajli, IEBC ikisema vifaa vya kupigia kura vitasambazwa siku ya Jumatano chini ya ulinzi wa maafisa wa polisi.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi