Mahakama ya Mombasa imeamuru washukiwa wanne wanaohusishwa na kusambaza taarifa za kupotea kwa sehemu za siri za wanaume kuzuiliwa kwa siku 10.
Washukiwa hao ni pamoja na David Moki Motonyi, George Otieno Ondiek, Sammy Chimvua na Idd Sudi Mohammed.
Katika ombi lililowasilishwa Mahakama na upande wa mashtaka, Maafisa wa upelelezi walikuwa wameomba washukiwa hao wazuiliwe kwa siku 14 ili kukamilisha uchunguzi wao, lakini Mahakama ikaagiza wazuiliwa kwa siku 10.
Polisi walidai washukiwa hao wanafaa kuchunguzwa zaidi kutokana na taarifa za uongo zilizozua hofu miongoni mwa wananchi ambazo zilisababisha mashambulizi kwa baadhi ya watu.
Polisi walisema matukio hayo ya mashambulizi dhidi ya watu kwa kisingizio cha sehemu za siri kupotea kumesababisha raia kuishi na wasiwasi licha ya wataalamu wa kiafya kuashiria masuala hayo na mambo ya kiafya na wala sio ushirikiana.
Washukiwa hao wanatarajiwa kurejeshwa Mahakama baada ya muda wa siku 10 kutokana na agizo la Mahakama ambapo maafisa wa upelelezi wa kesi hiyo wanatakiuwa kukamilisha uchunguzi wao kwa muda waliyoomba.
Taarifa ya Mwanahabari wetu
