Mahakama ya Kilifi imehairisha kesi ya unyakuzi wa ardhi Kilifi

Mahakama ya Kilifi imehairisha kesi ya unyakuzi wa ardhi Kilifi

Mahakama ya Kilifi imehairisha kesi inayomhusu mshukiwa wa unyakuzi wa ardhi ya thamani ya shilingi milioni 165 hadi tarehe 29 mwezi Mei mwaka huu.

Armando Tanzini ambaye ni raia wa Italia pamoja na wenzake ambao hakuwa Mahakamani wanadaiwa kunyakua ardhi ya nambari Chembe-Kibabamshe/408, mali ya marehemu Kitsao Mashobo Nyaki.

Katika kesi hiyo, Kiongozi wa mashtaka ya umma Ridhwan Mohammed aliieleza Mahakama kwamba mnamo mwezi Machi mwaka 1994, washukiwa hao walifanya usajili wa ardhi hiyo katika ofisi za usajili wa ardhi mjini Kilifi wakijifanya kuwa wameuziwa ardhi hiyo.

Mahakama ilimuachilia Armando kwa dhamana ya shilingi laki 2 pesa tasilimu na Mahakama ikaagiza kuzuiliwa kwa cheti chake cha usafiri (passport) ili kupata muda wa kuwaleta washukiwa wengine Mahakamani

Katika kikao cha siku ya Jumatatu tarehe 25 mwezi Mei mwaka huu Mahakamani, Armando aliomba Mahakama kumrudishia cheti chake cha usafiri baada ya washukiwa wengine kukosa kufika mahakamani tangu kesi hiyo ianze, japo Mahakama ikasengeze kesi hiyo hadi tarehe 29 mwezi huu.