Zoezi la upigaji kura katika eneo bunge la Emurua Dikkir linaendelea vyema katika vituo 94 vya kupigia kura na zoezi hilo linatarajiwa kutamatika mwendo wa saa kumi na moja unusu.
Zaidi ya wapiga kura 44,353 waliojisajiliwa wanaendelea kushiriki uchaguzi huo ili kumchagua kiongozi wanayemtaka baada ya aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Johanna Ng’eno kufariki katika ajali ya ndege mwezi Februari mwaka huu.
Wakaazi ambao tayari wameshapiga kura, walisema umeanza vyema tangu mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi na zoezi hilo linaendelea kwa amani na usalama wa hali juu, huku wakiwataka wenzao kujitokeza na kushiriki zoezi hilo la kidemokrasia.
“Tumejitokeza toka asubuhi saa kumi na moja kupiga kura kwa amani na tunamatumiani kwamba uchaguzi utakuwa huru na haki”, alisema wakaazi.

Wakaazi wa eneo bunge la Emarua Dikkir wanashiriki uchaguzi mdogo wa eneo bunge hilo
Afisa msimamizi wa IEBC eneo bunge hilo Caleb Gikonde alisema maafisa wa tume hiyo wamejiandaa vyema kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa njia huru na haki.
“Uchaguzi unaendelea vizuri katika vituo vyote 94 katika eneo hili la Emurua Dikkir. Tumejipanga vyema na uchaguzi unaendelea, kuhakikisha watu wanashiriki uchaguzi. Wale ambao wanakuja kupiga kura tunawahimiza kubeba vitambulisho vyao”,alisema Gokonde.
Uchaguzi hao hata hivyo umewavitia zaidi ya wagombea watano, akiwemo Vincent Rotich wa Chama cha DCP, David Keter wa UDA, Desma Cherono wa PNU, Gideon Koech wa NVPK na Ken Kiprono wa RLP.
