Vijana 70 wamekamatwa kufuatia msako wa Mawoza Kilifi

Vijana 70 wamekamatwa kufuatia msako wa Mawoza Kilifi

Kamishna wa kaunti ya Kilifi David Wanyonyi amethibitisha kuwa zaidi ya vijana 70 ambao wanahusishwa na makundi ya kihalifu wametiwa mbaroni katika msako ambao unaendelezwa na maafisa wa usalama katika maeneo mbalimbali ya kaunti ya Kilifi.

Akizungumza mjini Kilifi, Wanyonyi alisema kuwa idara ya usalama inaendelea kuyadhibiti magenge hayo kupitia mpango wa kujumuisha jamii katika kudumisha usalama unaowasaidia kupata taarifa kuhusu vijana hao.

‘’Tumekuwa na changamoto ya utovu wa usalama, sana sana tunaipata kwa jina ya ‘mawoza’. Hawa vijana wamekuwa wakisumbua wananchi na kama mwenyekiti wa usalama kaunti ya Kilifi tunaweka mikakati pamoja kuhakikisha hawa vijana wanakabiliwa vilivyo’’ alisema Wanyonyi

Kamishna wa kaunti ya Kilifi David Wanyonyi amethibitisha kukamatwa kwa zaidi ya vijana 70 ambao wanahusishwa na makundi ya kihalifu “Mawoza”, kaunti ya Kilifi

Wanyonyi alitaja maeneo ya Watamu, Mtwapa na baadhi ya vijiji eneo la Kilifi Kaskazini akisema ni miongoni mwa yale ambayo yameathirika zaidi kutokana na ukosefu wa usalama.

Taarifa ya Janet Mumbi