Baraza la makanisa nchini NCCK limetoa mapendekezo 7 kwa serikali za kaunti na serikali ya kitaifa, likitaka mapendekezo hayo kutekelezwa mara moja.
Kati ya mapendekezo hiyo ni pamoja na kuboreshwa kwa sekta ya Afya, kutatuliwa kwa vizozo ya ardhi, ukosefu wa maji, mzozo wa binadamu na wanyamapori miongoni mwa mengine.
Katika kikao na Wanahabari baada ya Kongamano la siku mbili lililoandaliwa mjini Kilifi na kujumuisha viongozi wa baraza hilo la NCCK tawi la Pwani, viongozi hao wamesisitiza haja ya kutatuliwa kwa masuala hayo 7.
Kongamano hilo ambalo pia lilichojumuisha Wawakilishi wa vijana na akina mama, limetaka suala tata la usalama kutatuliwa, kuboreshwa kwa sekta ya Afya, wakaazi kupewa hati miliki, pamoja na Mihadarati kukomeshwa Pwani.
Mwenyekiti wa baraza hilo kanda ya Pwani Askofu Peter Mwero amesema kama viongozi hawatarudi nyuma hadi masuala hayo kutetuliwa, akiweka wazi kwamba watahakikisha viongozi wa serikali za kaunti na kitaifa wanashirikishwa.
Viongozi hao wametaka suala la ukosefu wa usalama Pwani kuimarisha na idara ya usalama kuhakikisha inakabiliana kikamilifu na magenge ya wahalifu ya Mawoza na yale ya vipanga kaunti ya Kwale.
Mwakilishi wa akina mama katika baraza hilo kanda ya Pwani, Priscillar Moira amesisitiza haja ya serikali za kaunti kuliangazia suala la ukosefu wa maji, akisema imekuwa changamoto kubwa kwa wakaazi.
Mwakilishi wa vijana katika baraza hilo kanda ya Pwani Valerie Shali ameitaka Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kuhakikisha inajiandaa vyema kwa kuhakikisha wananchi wana imani na utendakazi wao, akiwataka pia vijana kujisajili kama wapiga kura.
