Taasisi ya utafiti wa matibabu nchini KEMRI limezindua mradi unaolenga kuchunguza athari za chembechembe ya simu ya Aflatoxin na athari za mabadiliko ya tabia nchi miongoni mwa watoto katika bara la Afrika maarufu TRACE.
Katika taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo, mradi huyo wa TRACE, ni kati ya mipango endelevu ya kudhibiti vifo na athari za kiafya, ikizingatiwa kwamba chembechembe za sumu ya Aflatoxin zina uwezo wa kusababisha saratani ya maini.
Hata hivyo wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo wakiwemo wa Wizara ya Kilimo nchini wamesisitiza haja ya mradi huo kupewa kipaumbele zaidi kwani mara nyingi sumu ya Aflatoxin hupatikana katika nafaka hasa Mahindi.

Watafiti na wadau wa masuala ya kiafya na maafisa wa serikali wakati wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa TRACE kaunti ya Kilifi
KEMRI, imeweka wazi kwamba nafaka kama Mahindi ni chakula ambacho kinatumika sana katika bara la Afrika, na kwamba mradi huo ambao utatekelezwa pia kaunti ya Kilifi utasaidia serikali kubuni sera ya kudhibiti ulaji wa vyakula vyenye Aflatoxin.
Daktari James Nyagwange ambaye ni mtafiti kwenye taasisi ya KEMRI , amesema Aflatoxin mara nyingi hujifika katika makaazi ya jamii za afrika kutokana na nafaka wanazozalisha hasa Mahindi na Njugu.
Tayari serikali ya kaunti ya Kilifi imebuni sera maalum itakayohakikisha chakula kinachozalishwa mashinani hakina chembechembe za Aflatoxin.
Taarifa ya Janet Mumbi
