Idara ya utabiri wa hali ya hewa kanda ya Pwani imetoa tahadhari ya kushuhudiwa kwa mvua kubwa, kuanzia wiki ijayo ya milimita 20 kwa saa 24.
Idara hiyo imezitaja kaunti za Pwani ikiwemo Kwale, Mombasa, Kilifi, Tanariver na Lamu kwamba zitashuhudia mvua hizo pamoja na kusababisha mafurikio, ikiwataka wananchi kuwa waangalifu.
Maeneo yalitojwa kushuhudia mafuriko ni pamoja na eneo la Sultan Hamud, kwenye barabara kuu ya Mombasa-Nairobi, eneo la daraja ya Mbogolo kwenye barabara kuu ya Mombasa-Malindi pamoja na maeneo ya Likoni na Nyali kaunti ya Mombasa.
Wakaazi wanaoishi katika maeneo ya nyanda za chini katika kaunti ya Tanariver na Kwale wahimizwa kuhamia maeneo salama ili kuepuka majanga sawa na kuzingatia mazingira salama na safi.
Wakati huo huo idara hiyo imewashauri wananchi wanaoishi karibu na Mto Tana katika kaunti ya Tanariver kuchukua tahadhari ya mapema na kuhamia maeneo salama kwani huenda mto huo ukavinja kingo zake.
Hata hivyo Afisa wa Mawasiliano wa Kampuni ya usambazaji maji ya GAWASCO katika kaunti hiyo, Omar Abdullahi alisema huenda wakaazi wa kaunti hiyo wakabiliwa na uhaba wa maji kufuatia mafuriko.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi
