Marehemu Mary Mutisya hatimaye wazikwa kijiji cha Tezo, Kilifi

Marehemu Mary Mutisya hatimaye wazikwa kijiji cha Tezo, Kilifi
Kijiji cha Tezo eneo bunge la Kilifi Kazkazini kaunti ya Kilifi hali ilikuwa tofauti kwa familia ya Marehemu Mary Mutisya baada ya kuzuka mvutano wa kifamilia na kusababisha marehemu kusalia kwenye makafani ya hospitali kuu ya rufaa ya Kilifi kwa zaidi ya miezi 11.
Familia hiyo ilidai kwamba ilikuwa ikihangaishwa shangazi wao kutokana na umiliki wa ardhi wanaoishi ya zaidi ya ekari 24 katika kijiji hicho ambayo waliachiwa na baba yao ambaye kwa sasa ni marehemu pia.
Kulingana na familia hiyo ikiongozwa na Morgan Mwamuye, tangu kifo cha mamake mzazi mwezi Aprili 15, 2025 juhudi za kumzika zimekuwa zikgonga mwamba kutokana na shangazi zao kuzuia mazishi hayo kupitia kesi Mahakamani.

Familia yaomboleza kifo cha Mary alifariki tangu mwezi Aprili 15, 2025 na kusalia Mochari kwa kipindi cha miezi 11

Mwamunye aliasema licha ya kuchimba kaburi la mama yao, kuburi hilo lilifunikwa kutokana na agizo la Mahakama baada ya shangazi wa vijana hao kuwasilisha kesi Mahakamani, kwa misingi kwamba ardhi hiyo ni mali ya familia kuu na wala sio ya watoto wa marehemu, mvutano ambao ulidumu kwa muda mrefu.
“Sisi tumeishi kwa ardhi hii tangu tuko wadogo na hii nyumba hapa ilijengwa na kakangu mkubwa na akamuhamisha mama hapo na hatujakuwa na shida na shangazi zetu lakini sasa tunashangaa hawataki tumzike mama na hii shamba alitengeneza mama na kupanda miti na miembe hata minazi lakini leo tunahangishwa na shangazi zetu ni haki kweli?”, alisema Morgan mtoto wa Marehemu.

Mwili wa Marehemu Mary Mutisya hatimaye wazikwa kijiji cha Tezo, Kilifi

Morgan alisema kwamba kifo cha mamake kilikuwa cha kutatanisha kwani aliugua kwa muda mfupi na mguu wake ulikuwa umevimba na kutokwa maji kila mara hali iliyopelekea kifo chake. Licha ya kuwa na ufahamu wa kilichokuwa kikiendelea mamake mzazi hakupata msaada wowote.
Kwa upande wake, Raymond Mwamuye ambaye pia ni mtoto wa Marehemu alisema licha ya kuomba kupewa ruhusu kumzika mama yao bado ilikuwa changamoto kwani waliwahi kuchimba kaburi kwa mara tatu bila ya kupata idhini ya kumzika mama yao kwani maafisa wa usalama walikuwa wakilinda eneo hilo.
Aidha alisema shangazi zake ndio waliokuwa mstari wa mbele kuwapokonya ardhi yao na hata kuzuia familia yao kumzika mama yao, wakilenga kuuza ardhi hiyo.
Mzee Chai Anderson ambaye ni jirani wa familia hiyo ya Marehemu alisema haki ya familia ya marehemu inafaa kuzingatiwa na wala sio kuhangaisha kila mara akipendekeza serikali na viongozi kuingilia kati suala hilo kuinusuru familia hii.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi