Mahakama ya Kilifi imemhukumu kifungo cha miaka 31 gerezani Collins Hamis baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi mtoto mwenye umri wa miaka 16.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo Charles Obulusta baada ya ushahidi kuwasilishwa Mahakamani.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Obulutsa amesema hukumu hiyo itakuwa funzo kwa watu wenye tabia kama hizo katika jamii.
Awali upande wa mashtaka ulieleza Mahakama kwamba mnamo tarehe 16 mwezi Machi mwaka 2025 katika eneo la Chumani, eneo bunge la Kilifi kazkazini kaunti ya Kilifi, masaa ya usiku Collins alimvuta kwa nguvu mlalamishi akiwa ametoka Disco matanga na rafiki yake na kumsukuma hadi kwa kichaka alipokuwa amejificha na kuetekeleza kitendo hicho cha kimya cha kumnajisi na kumlawiti kisha kumtishia kumuua akiwa na panga.
Hakimu Obulutsa aidha alikemea vikali tabia za vijana wa bodaboda kuwadhulumu kingono watoto hususani katika sherehe za disco matanga, akiongeza kwamba suala la disco matanga limekuwa changamoto kubwa kaunti ya Kilifi hata baada ya serikali kupiga marufuku sherehe za disco matanga ambazo huchangia wasichana wadogo kudhulumiwa, bado zinaendelea kisiri.
Aidha Collins ameagizwa kuwa na siku 14 za kukata rufaa andapo hakuridhishwa na hukumu hiyo.
Taarifa ya Teclar Yeri.
