Idara ya misitu kaunti ya Kwale imesema kiwango cha misitu kimefikia asilimia 13.9, ikisisitiza kwamba bado kiwango hicho kiko chini mno ikilinganishwa na kiwango cha miti kinachohitajika.
Afisa wa idara hiyo katika kaunti ya Kwale Elvis Fondo, alisema lengo la mpango huo ni kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2032, akibainisha kwamba juhudi zinaendelea kuimarishwa ili kuongeza upandaji miti.
Akizungumza katika eneo la Shimba Hills, Fondo aliwahimiza wakaazi kutumia msimu huu wa mvua kupanda miti kwa wingi, ikiwemo miti ya matunda ili kuchangia usalama wa chakula.
“Bado hatujafikia kiwango kinachohitajika tuko katika asilimia 13.9 ya miti na lengo letu ni kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka wa 2032 ili kuhakikisha
Kwa upande wake Afisa wa mazingira kutoka Shirika la WEWORLD, John Ely, alitoa wito kwa wananchi kutunza mazingira, hasa kwa kudhibiti na kukusanya taka za plastiki ili kupunguza uchafuzi wa mazingira.
Taarifa ya Mwanahabari wetu
