Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imesema kufikia sasa, imesajili wakenya 250, 391 na kufikia idada ya wakenya waliosajili kuwa 22,352,923.
Kamishna wa Tume hiyo Alutalala Mukhwana alisema idadi hiyo inajumuisha asilimia 50.9 ya wanaume na asilimia 49.1 ikiwa na wanawake huku asilimia 67.35 ikiwa na wale wa umri wa miaka 35 na zaidi huku asilimia 32 ikiwa wale wa chini ya miaka 35.
Alutalala alisema idadi hiyo inaonyesha wazi kwamba usajili wa vijana kama wapiga kura iko chini mno, akisisitiza haja ya vijana kujitokeza kwa wingi kupitia shinikizo la Niko Kadi na kusajili idadi kubwa ya wapiga kura.
Aidha alidokeza kwamba japo baadhi ya wakenya wametambua haki ya upigaji kura kupitia hamasa mbalimbali, wengi wanaojitokeza na wale wanaoishi katikati ya miji mikuu, akiwarai wananchi walio vijiji pia kujisajili.
Wakati huo huo alidokeza kwamba ili Tume ya IEBC iandea uchaguzi huru, haki na usawa ni lazima, maafisa na makamishna wa tume hiyo wapewe mazingira bora ya kujiandaa na wala sio wanasiasa na wananchi kuikosoa tume hiyo kila mara.
“Ili kufanikisha uchaguzi huru haki na usawa ni lazima tupewe mazingira safi, salama na yenye amani kwa sababu kuandaa uchaguzi sio jambo rahisi kwani linahitaji mikakati bora lakini hapa kwetu sio wanasiasa ama wananchi wako na fikra tofauti kabisa kwa sisi maafisa wa IEBC”, alisema Alutalala.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi
