Mahafala baharini wahitimu kwa ujuzi mbalimbali

Mahafala baharini wahitimu kwa ujuzi mbalimbali

Kiwango cha mashindano ya kila mwaka ya mbio za jahazi ambayo huandaliwa katika mkono wa bahari wa Old Ferry mjini Kilifi.

Mwenyekiti wa bodi ya Hazina ya ustawi wa michezo na sanaa Wakili George Kithi ambaye pia ni mgombea wa wadhfa wa Seneta kaunti ya Kilifi amesema mashindano hayo sasa yatapanda hadhi na kuwa tukio la kimataifa litakalowaleta washiriki kutoka kote duniani na kulifanya kivutio cha kiutamaduni na baharini kinachovuka mipaka ya taifa

Akizungumza katika hafla ya kipekee ya kuwakabidhi vyeti vya kuhitimu mahafala 68, baada ya kukamilisha mafunzo ya wiki mbili kuhusu mbinu za kuishi baharini, uokoaji majini na upigaji mbizi wa (scuba diving), Wakili Kithi ametaja kuwa Mafunzo haya yamewapa vijana ujuzi wa kukabiliana na hatari majini, kutoa huduma ya kwanza, kujitetea na mbinu za ubaharia.

Aidha Wakili Kithi alisisitiza dhamira yake ya kuinua miradi ya Kilifi hadi viwango vya kimataifa kupitia hazina ya Michezo, Sanaa na Maendeleo ya Kijamii.

Mafunzo haya yenye manufaa makubwa yaliendeshwa na Shirika la Coast Sea Survival kwa ushirikiano na Kikosi cha Masuala ya Kiraia cha Jeshi la Wanamaji la Marekani, yakilenga kuwapa vijana stadi muhimu za kuokoa maisha na kujiendeleza katika sekta ya baharini.

Kithi alisema Kwamba Kupitia ruwaza yake atahakikisha Bahari si tu chanzo cha riziki, bali pia ni daraja la matumaini na fursa mpya kwa vijana wa pwani.

Taarifa ya Lolani Kalu