Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC inanuia kuongeza vituo vya kupigia kura hadi 55,393 katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 kutoka vituo 46,229 mwaka wa 2022.
Vituo vya kupigia kura vilivyoongezwa ni 9,169 huku idadi ya wapigaji kura katika kila kituo ikisalia 700.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, kupitia Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon, tume hiyo inalenga kusajili wapiga kura wapya milioni 6 kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Tume hiyo ilisema vifaa vya kupigia kura vya Kiems Kits 45,352 vitabadilishwa kwa gharama ya shilingi bilioni 6 kwani havifanya kazi tena huku vifaa vingine elfu 14 vikifanyiwa marekebisho zaidi kwa gharama ya shilingi elfu 175 kwa kila kifaa.
Hata hivyo pendekezo hilo linasubiri bunge la kitaifa kuliidhinisha ili kuiwezesha tume ya IEBC kujiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi
