News

Ndoto ya Matiang’i kuwania urais 2027 yaingia doa

Published

on

Mbunge wa Gem Elisha Odhiambo ametangaza mipango ya kumchukulia hatua za kisheria aliyekuwa waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i kutokana na madai ya mauaji ya kiholela wakati wa utawala wa serikali ya Jubilee.

Mbunge huyo alifichua kuwa anakamilisha ombi la kutaka kumzuia Dkt. Matiang’i kuwania urais, akimwajibisha kwa kile alichokitaja kama dhuluma zilizoidhinishwa na serikali – haswa kutupwa kwa miili katika Mto Yala.

“Kama mbunge wa Gem, nilifanya mkutano na mawakili jana usiku baada ya kusikiliza kauli ya Matiang’i akithibitisha kuwa Wakenya kadhaa waliouawa kwa kuchinjwa walitupwa kwenye mto Yala, tunaenda katika mahakama ya rufaa ili tuweze kumshtaki kama mtu binafsi kwa miile kutupwa kwenye mto Yala ili awajibike kama afisa wa zamani wa afisi ya usalama wa kitaifa,” ilisema Odhiambo.

Odhiambo alimshutumu waziri wa zamani wa mambo ya Ndani kwa kusimamia utawala wa ugaidi uliosababisha uharibifu wa mazingira na kibinadamu katika baadhi ya maeneo ya eneo bunge la Gem.

Alidai kuwa miili mingi iligunduliwa ikiwa imetupwa katika mto Yala wakati wa uongozi wa Matiang’i, akitaja tukio hilo kama “ugaidi wa mazingira” na doa kwa ustawi wa jamii.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee na runinga moja nchini siku ya Jumanne mwezi juni 2, 2025, Matiang’i alisema alifuatilia suala la miili ya River Yala kwa Inspekta Jenerali wa polisi wakati huo Hillary Mutyambai, ambaye alishikilia kuwa walihitaji familia hizo kutambua miili hiyo ili kufichua ukweli.

Taarifa ya Joseph Jira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version