News
NACADA: Idadi kubwa ya vijana imeathirika na Mihadarati
Changamoto imetolewa kwa idara ya usalama, bodi ya kukabiliana na utumizi wa pombe haramu sawa na dawa za kulevya kuwajibika kikamilifu kwa lengo la kukabiliana na uraibu huo.
Kwa mujibu wa maafisa wa NACADA eneo la pwani, imebainika kuwa uraibu wa pombe haramu sawa na dawa za kulevya ikiwemo Heroine na bangi unaendelea kushamiri kwa kasi miongoni mwa vijana hali wanayodai inahatarisha kizazi kijacho.
Wakizungumza eneo la Kaloleni kaunti ya Kilifi, maafisa hao walisema kuna haja ya asasi za kiusalama kushirikiana ili kukomesha uraibu huo kwani asilimia mkubwa ya vijana wanaendelea kuathirika.
Wakati huo huo waliwalaumu baadhi ya wafanyabiashara wa vileo wakiwataja kama wanaokiuka sheria kwa kuendeleza biashara bila ya kufanyiwa ukaguzi, wakisema kwamba hatua za kisheria dhidi yao zitachukuliwa.
Taarifa ya Mwanahabari wetu.