News

NACADA kushirikiana na Polisi kudhibiti Mihadarati

Published

on

Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya kukabiliana na mihadarati na vileo haramu nchini NACADA tawi la kaunti ya Taita Taveta Anthony Kiseu ametoa wito kwa asasi za usalama kushirikiana na NACADA  ili kudhibiti ulanguzi wa dawa za kulevya.

Kiseu alisema katika kaunti ya Taita Taveta, idadi ya wanaokunywa pombe haramu, kuvuta bangi na Heroin imeongezeka.

Aidha, Kiseu alisema ni kupitia ushirikiano huo ndipo wataweza kuwanusuru vijana ambao ni waraibu wa pombe haramu na mihadarati.

“Kama sehemu ya Voi muda mwingi mzigo ukitoka Nairobi ama sehemu zingine lazima upite hapa ukielekea Mombasa’’ alisema Kiseu.

Wakati huo huo alielekeza kidole cha lawama kwa baadhi ya wamiliki wa maeneo ya kuuza vileo kwa kuendeleza biashara hiyo bila kuwa na vibali.

“Kama hii sehemu ya Birikani hapa tumekuta kuna baa zaidi ya tano, ambazo hizo baa ziko wazi usiki na hazina vibali’’ aiongeza Kiseu.

Vilevile, alisema ni lazima wanaofanya biashara hiyo kinyume cha sheria wakamatwe na wakabiliwe ipasavyo.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version