News
Mwaro, Azuiliwa Kuingia Ofisini
Kumeshuhudiwa vuta ni kuvute katika Ofisi za Katibu wa kaunti ya Kilifi baada ya aliyekuwa Katibu wa kaunti Martin Mwaro kupata agizo la Mahakama la kurejea kazini.
Vurugu hizo zimesababisha Katibu huyo kutoingia ofisini mwake baada ya kufurushwa na kundi la vijana waliyoongozwa na Kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya Kilifi Ibrahim Matumbo.
Hata hivyo Ofisi ya Katibu huyo imesalia kufungwa hali ambayo imechangia sintofahamu huku wananchi wakishangazwa na tukio hilo.
Haya yamejiri baada ya Mwaro wiki iliyopita kufutwa kazi na Gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Mung’aro kwa madai ya utendakazi duni na ukosefu wa uadilifu.