International News
Musevani ateuliwa kuwania urais Uganda mwaka 2026
Chama tawala nchini Uganda, cha National Resistance Movement (NRM), kimemteua Rais Yoweri Museveni kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2026.
Akizungumza baada ya uteuzi huo uliofanyika katika makao makuu ya Tume ya uchaguzi ya chama cha NRM mjini Kampala, Rais Museveni alisema atazingatia zaidi masuala ya kuinua uchumi wa jamii na maendeleo.
Museveni alisema iwapo atachaguliwa tena kuliongoza taifa hilo basi atahakikisha Uganda inaendelea kushuhudia maendeleo licha ya kutawala taifa hilo kwa zaidi ya miaka 40 tangu mwaka wa 1986.
Japo taifa la Uganda limekuwa likiandaa chaguzi za kidemokrasia, Rais Museveni alishtumiwa kwa kukandamiza upinzani na kuendeleza utawala wa kidikteta.
Museveni na mkewe Janet wakiwasili katika makao makuu ya NRM
Akiwa uingozini, Rais Museveni alishinikiza kufanyika kwa mabadiliko Katiba ya nchi hiyo, kwanza mnamo mwaka wa 2005 kuondoa umri unaoruhusu mtu kuwania kiti cha urais nchini humo na kisha mnamo mwaka wa 2017, katiba hiyo ikafanyiwa marekebisho kufutiliwa mbali vipindi vya kiutawala.
Kufuatia hatua hiyo, sasa Museveni ana nafasi nzuri ya kuwania tena kiti cha Urais mwaka ujao wa 2026 wakati w auchaguzi mkuu nchini humo.
Upinzani ulishtumu vikali hatua hiyo ukisema ni ukiukaji wa Katiba huku Mpinzani mkuu nchini humo Kizza Besigye yuko korokoroni akikabiliwa na shtaka la uhaini ingawa hali yake ya afya inatajwa kuendelea kudhofika.
Taarifa ya Eric Ponda