Sports
Liverpool Yakubaliana Dili Ya Kerkez
Kilabu ya Liverpool imekubaliana na AFC Bournemouth kuhusiana na uhamisho wa pauni milioni 4o kwa beki Milos Kerkez raia wa Serbia.
Tineja huyo anatarajiwa kuwasili Liverpool muda wowote kufanyiwa vipimo vya kimatibabu na kumwaga wino mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa ligi kuu Uingereza.
Mchezaji huyo alikua nguzo muhimu kwa kilabu ya Bournemouth wakimaliza kumi bora akichangia magoli matano na kufunga mawili,anakua sajili wa tatu kwa kocha Arne Slot kwenye kilabu hio.
The Reds wakiwa wametumia pauni milioni 116 kumpata kiungo Florian Wirtz,pauni milioni 31 kupata Jeremie Frimpong.