Sports
Kocha Wa Stars Mccarthy Ataja Kikosi Cha Mwisho Kombe La CHAN
Mkufunzi wa timu ya soka Harambee Stars Benni Mccarthy amekitaja kikosi chake cha mwisho chenye wachezaji 25 tayari kwa kombe la Chan mwezi ujao,vijana wa nyumbani wakifungua dimba dhidi ya DR.Congo Agosti 3 ugani Kasarani.
Miongoni mwa nyota waliojumuishwa kikosini ni pamoja na kipa mzoefu wa kilabu ya Bandari FC Faruk Shikhalo,beki wa Police Aboud Omar ambaye atakua nahodha wa kikosi hicho pamoja na viungo Austine Odhiambo,Marvin Nabwire na mshambulizi Masoud Juma ataongoza safu ya mashambulizi pamoja na Ryan Ogam wa kilabu ya Tusker Fc.
Magolikipa;
Faruk Shikhalo, Byrne Omondi, Sebastian Wekesa
Mabeki;
Siraj Mohammed, Manzur Suleiman, Pamba Swaleh, Abud Omar, Alphonce Omija, Sylvester Owino, Mike Kibwage, Daniel Sakari, Lewis Bandi, Kevin Okumu
Viungo;
Brian Musa, Alpha Onyango, Austin Odhiambo, Ben Stanley, Marvin Nabwire
Washambulizi;
Mohammed Bajaber, Boniface Muchiri, David Sakwa, Ryan Ogam, Masoud Juma, Austin Odongo, Felix Oluoch
Stars wako kundi A pamoja na Angola,DR.Congo,Morocco na Zambia.