News
KNUT Yaitataka TSC kutekeleza CBA wa mwaka, 2025/2029
Naibu Katibu mkuu wa Chama cha kutetea maslahi ya walimu nchini KNUT Hesbon Otieno aliitaka Tume ya kuajiri walimu nchini TSC kuyapa kipau mbele mazungumzo ya makataba wa makubaliano wa malipo nchini CBA wa mwaka wa 2025/2029.
Hesbon alisema suala hilo linafaa kuchukuliwa kama la dharura, akimtaka Kaimu Afisa mkuu mtendaji wa Tume hiyo Evaleen Mitei kuhakikisha suala hilo linatekelezwa kwani CBA ya sasa haina manufaa yoyote ya kifedha kwa walimu.
Akizungumza katika kaunti ya Kericho, Hesbon alisema KNUT inadai ongezeko la asilimia 60 ya mishahara na ongezeko la asilimia 30 kama marupurupu kwa walimu wote nchini, akisisitiza haja ya ongezeko hilo la mshahara kutekelezwa.
“Tulifanya mazungumzo na TSC kwa muda mrefu na kuafikia nyongeza ya asilimia 60 ya mishahara kwani ile CBA ya sasa inaisha Juni na haina manufaa kwa walimu, ndio maana tunaiambia TSC itekeleza makubaliano ya CBA”, alisema Hesbon.
Itakumbukwa kwamba viongozi wa KNUT na TSC waliwahi kuwa katika mazungumzo ya zaidi ya mwaka mmoja na iwapo yatatekelezwa basi changamoto zinazowakumba walimu zitapungua.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi