News

KNCHR:Watu 31 walifariki kwenye maandamano ya Saba Saba

Published

on

Tume ya kutetea haki za binadam nchini KNCHR imetoa takwimu zikionyesha watu 31 wamefariki huku wengine 107 wakijeruhiwa kufikia sasa kufuatia maandamano ya siku ya Saba Saba ya siku ya jumamtatu juma hili.

Tume hiyo pia ilibainisha kuwa watu wawili walitekwa katika njia tatanishi huku wengine 532 wakikamatwa na polisi sehemu mbali mbali nchini.

KNCHR pia ilitaja kushuhudiwa kwa uharibifu mkubwa wa mali japo thamani yake bado haijabainishwa.

Katika taarifa yake makamu mwenyekiti ya tume hiyo Daktari Raymond Nyeris aliaani ukiukaji wa haki za binadam huku akishinikiza uwajibikaji kwa waliohusika wakiwemo polisi, raia na wadau wengine.

Tume hiyo pia ilituma risala za rambi rambi kwa waliofiwa na kuwapa pole majeruhi, huku ikisema inaendelea kufuatilia matukio yote yanayotokana na siku ya Sabasaba.

Taarifa ya Joseph Jira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version