Sports

Gwiji wa Tae-kwon-do Master Kihurani Asherekewa

Published

on

Gwiji wa mchezo wa tae-kwon-do mwanadada Caroline Wairimu Kihurani ambaye aliaga dunia wiki jana jijini Nairobi anazidi kusherehekewa na wengi kutokana na mchango wake mkubwa katika mchezo huo nchini baada ya kukuza vipaji vingi.

Mchezaji huyo aliingia kwenye daftari za kumbukumbu kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwakilisha Kenya katika mashindano ya dunia ya mchezo huo mwaka 1997 makala ya World Taekwondo Championships mjini Hong Kong Uchina.

Katika ibada ya wafu iliofanyika hapo jana wengi hawakusita kumiminia sifa kedekede mwendazake ambaye aliaga dunia na miaka 57 wakimtaja alikua shujaa kwenye mchezo huo.

Kulingana na Rais wa KTF Major Suleiman Sumba amesema kwamba gwiji huyo hatakumbukwa tu kwa kipaji chake bali pia kwa mchango wake kuwapa msukumo mtoto wa kike.

“Coach Carol kama alivyofahamika hatakumbukwa tu kwa ubora wake uwanjani na kipaji aliyokua nayo kwenye mchezo huu bali pia nyoyo za watoto wengi wa kike ambazo aliwapa nafasi kushiriki mchezo wa tae-kwon-do.

Mwendazake atapumzisha katika makao yake ya milele kule Ol-Joro-Orok siku ya Alhamisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version