News

Gachagua: Upinzani hauna nia ya kupindua serikali

Published

on

Aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua amekanusha madai kwamba mrengo wa upinzani unapanga kumuondoa rais William Samoei Ruto madarakani.

Katika taarifa yake ya siku ya Jumatano terehe 9 mwezi Julai, 2025 kwa vyombo vya habari, muda mfupi baada ya hotuba ya rais Ruto, Gachagua alisema vuguvugu la ONE TAM halina nia ya kuchukua mamlaka kwa njia ambayo sio halali.

Gachagua alimtaka rais Ruto kutekeleza majukumu yake ipasavyo na pia kudhibiti visa vya vya watu kutekwa nyara na kuuliwa katika mazingira tatanisha.

Gachagua pia alimkosoa rais Ruto akisema amekuwa akipuuza kilio cha wananchi hali ambayo inawafanya Wakenya wengi kuendelea kuhangaika.

‘’Bwana Ruto punguza hasira na kwa unyenyekevu mwingi nakushauri kwamba hasira sio suluhu maana haitakusaidia. Unapaswa kujua nini unapaswa kufanya maana haujakuwa ukiwasikiza Wakenya’’ alisema Gachagua.

Wakati huo huo, Gachagua ambaye pia ni Kinara wa chama cha DCP aliibua madai kwamba Rais Ruto amekuwa akiwatumia wahalifu kuharibu mali ya watu wakati maandamano ya vijana wa kizazi cha Gen Z ambao wamekuwa wakiandamana nchini kuwasilisha matakwa yao kwa serikali.

‘’Siku ya Sabasaba wahalifu hao walipeleka maandamano maeneo mbalimbali nchini hasa eneo la Mlima Kenya na yale mengine ambayo yanakashifu uongozi wa serikali kuu’’ aliongeza Gachagua.

Taarifa ya Janet Mumbi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version