News
Bunge la kitaifa limepitisha mswada wa fedha wa mwaka 2025
Bunge la kitaifa limepitisha mswada wa fedha wa mwaka wa 2025 ambao utaipa nafasi serikali ya Kenya kwanza kutekeleza majukumu yake kwa kuambatana na sheria.
Bunge hilo linatarajiwa pia kuwasilisha nakala za mswada huo kwa rais William Ruto ili kutia saini na kuwa sheria huku baadhi ya vipingele tata kwenye mswada huo vikifutiliwa mbali na bunge hilo.
Katika kikao cha bunge hilo kilichoongezwa na Spika Moses Wetangula kimekuwa na mdahalo mkali bungeni hatua ambayo ilipelekea kufutiliwa mbali kwa pendekezo lenye utata la kuipa Mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini KRA kufikia data za kibinafsi za kifedha za wananchi za kulipa kodi.
Mwenyekiti wa kamati ya fedha katika bunge la kitaifa ambaye pia ni bunge wa Molo Kuria Kimani, ilibainisha kwamba baada ya kutafakari walihitimisha kwamba kipengele kilichoiruhusu KRA kupata data za kibinafsi za kifedha za wakenya kilikiuka kifungu cha 31 {c} na {d} cha Katiba ya Kenya.
Itakumbukwa kwamba Waziri wa Fedha nchini John Mbadi alikuwa akitetea mara kwa mara hatua hiyo kama hatua muhimu katika kuboresha uzingatiaji wa ushuru.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi