Business

Afueni kwa wakulima wa Pamba Lamu

Published

on

Wakulima wa zao la pamba kaunti ya Lamu wamepata afueni baada serikali kujengewa kiwanda cha kutayarisha zao la pamba.

Katibu katika idara ya uekezaji kaunti hiyo Abubakar Hassan alisema kuwa mpango huo unalenga kugatua ustawi wa viwanda na kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka mataifa ya kigeni.

Akizungumza na vyombo vya habari Hassan alisema kuwa kiwanda hicho kinatarajiwa kuwapa fursa za masoko wakulima wa zao hilo kikiwa sehemu ya mpango wa serikali kufungua viwanda nyanjani.

Katibu huyo aliongeza kuwa kupitia mpango huo serikali inalenga kuwawezesha wakulima wa zao hilo na kuboresha uchumi wa wakulima hao na kaunti kwa ujumla.

Taarifa ya Pauline Mwango

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version