News
Gavana Mung’aro awaonya wanaoishi karibu na matimbo kaunti ya Kilifi
Serikali ya kaunti ya Kilifi imewaonya watu wanaoishi karibu na Timbo iliyoporomoka jana na kusababisha maafa kutoingia katika timbo hilo ili kudhibiti visa vya watu kufariki.
Akizungumza na wanahabari gavana wa kaunti ya kilifi Gedion Mung’aro amesema serikali ya kaunti ya Kilifi itaweka maafisa watakaohakikisha hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kuingia katika eneo hilo.
Mung’aro amebainisha kuwa shughuli za uokozi zingali zinaendelea huku waathiriwa wakiendelea kupokea ushauri katika hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi kaunti hii ya Kilifi.
Hata hivyo gavana Mung’aro amebainisha kuwa serikali yake itabuni mbinu mbadala za kuwawezesha kiuchumi wakaazi wanaojihusisha na shughuli zinazohatarisha maisha yao ili kujikimu kimaisha.