News

Uchaguzi wa Papa Mpya Kuanza Mei 7

Published

on

Ofisi ya Vatican imetangaza kwamba Baraza la Makadinali wa Kanisa Katoliki linalofahamika kama ”Conclave” litaanza kikao chake cha siri cha kumchagua Papa mpya kuanzia tarehe 7 mwezi Mei.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Vatican, uamuzi wa kuanza kwa mchakato huo uliafikiwa katika kikao cha faragha cha makadinali kilichofanyika Vatican, kikao cha kwanza tangu mazishi ya Papa Francis yaliyofanyika siku ya Jumamosi.

Kikao hicho cha siri kitafanyika ndani ya Kanisa la Sistine, ambalo litafungwa kwa kipindi chote cha uchaguzi huo wa kihistoria.
Jumla ya makadinali 135 kutoka mataifa mbalimbali wote wakiwa na umri wa chini ya miaka 80 watashiriki katika mchakato huo wa kumchagua Papa mpya wa Kanisa Katoliki lenye waumini zaidi ya bilioni 1.4 kote duniani.
Hata hivyo ulimwengu sasa unaelekeza macho Vatican, ikisubiri kwa hamu kutangazwa kwa kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version