News

Liverpool Mabingwa Mara 20 Epl

Published

on

Sasa Ni rasmi kwamba kilabu ya Livrpool ndiyo mabingwa wa Ligi kuu Uingereza baada ya kuvuna ushindi mnono wa magoli 5-1 dhidi ya Tottenham Hotspurs Ugani Anfield.

Mshambulizi Dominik Solanke aliwaweka uongozini dakika ya 12 kabila ya mshambulizi Luis Diaz kuisawazishia vijana wa kocha Arne Slot kunako dakika ya 16. Kiungo Alexis Mc Allister aliweka kambani chuma ya pili dakika 24 kabila ya winga Cody Gakpo kuweka goli la tatu dakika ya 34.

Goli la nne lilitiwa kimyani na mshmabulizi nyota Mohammed Salah dakika ya 63. Huku Goli la Tano likitiwa nyavuni kwa kujifunga kutoka kwa beki wa Spurs Destiney Odogie.

Ushindi huu ukiipa The Reds alama 82 kileleni baada ya mechi 34 huku kilabu ya Arsenal ikifuata nafasi ya pili na alama 67 nao Newcastle United ikiwa ni ya tatu na alama 62 ,mancity ni ya nne na alama 61 Huku Chelsea akifunga tano bora na alama 60

Vilabu vya Southampton,Leicester city na Ipswich Town vyote vikishushwa ngazi ligi hio navyo Leeds United na Burnley tayari zimejikatia tiketi ya kurejea Epl baada ya kuongoza ligi ya Championship na alama 84.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version