News
Fikirini, Ameapishwa Rasmi kuwa Katibu katika Wizara ya Michezo na Vijana
Rais William Ruto ameshuhudia kuapishwa kwa mawaziri wawili wapya pamoja na makatibu katika Wizara mbalimbali nchini katika halfa iliyoandaliwa katika Ikulu ya Nairobi.
Wakati wa halfa hiyo, mawaziri na makatibu hao wameapa kuwajibikia majukumu yao kikamilifu kwa kuzingatia kanuni za nchi sawa na kuheshimu muongozo wa Katiba.
Geoffrey Ruku aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Utumishi wa umma nchini pamoja na Hanna Cheptumo kama Waziri wa jinsia wameapishwa rasmi kuanza majukumu yao ya kikazi.
Wengine walioapishwa ni makatibu katika Wizara mbalimbali baada ya kuidhinishwa na bunge la kitaifa ambapo Fikirini Jacobs kama Katibu katika Wizara ya Michezo na vijana, Caren Achieng Ageng’o, Aden Abdi Mila miongoni wa wengine wameahidi kutumikia taifa kikamilifu.
Akizungumza baada ya kuapishwa kwa mawaziri na makatibu hao, Rais William Ruto amewashauri mawaziri na makatibu hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamalifu ili kufanikisha malengo ya wananchi.