News
Wanafunzi Watatu Wazama Maji Kisiwani Lamu
Maafisa wa uokozi wanaendelea na juhudi za kusaka miili ya vijana watatu ambao ni wanafunzi kutoka eneo la Hongwe Mpeketoni waliozama baharini siku ya Jumapili jioni katika eneo la Shela Kisiwani Lamu.
Watatu hao walikuwa miongoni mwa vijana zaidi ya 20 pamoja na Mwalimu wao wakati wakiogelea kabla ya baadhi yao kuokolewa.
Wanafunzi waliozama baharani wana umri wa miaka 14 na 18 ambao ni wanafunzi wa shule ya upili, huku mmoja akiwa na umri wa miaka 24 akiwa amekamilisha masomo ya kidato cha nne.
Maafisa wa kitengo cha Coast Guard katika kaunti ya Lamu wamesema vijana hao pamoja na wasimamizi wao walikuwa wametoka Kanisani kisiwani Lamu na kuelekea Shela kujivinjari kabla ya watatu hao kukumbwa na mkasa huo.
Maafisa hao wamesema kumekuwa na mawimbi makali baharini.