News

Askofu Lagho: Marufuku Siasa Kanisani

Published

on

Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo mkuu la Malindi Willybard Lagho, ametoa onyo kali kwa viongozi wa kisiasa dhidi ya kutumia vibaya Kanisa na kuendeleza maswala ya kisiasa na utakatishaji fedha.

Askofu Lagho amesema Kanisa hilo halitakubali viongozi wa kisiasa kulitumia vibaya kwa manufaa yao binafsi, akisisitiza haja ya wanasiasa kuheshimu sehemu za Ibada.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Askofu Lagho amesema mwanasiasa yeyote atakayemujulisha kiongozi wa kanisa kuhusu mipango yake na ibada maalum atakazoshiriki Kanisani hafai kutambulishwa Kanisani.

Askofu Lagho amewaonya mapadre na viongozi wa makanisa katoliki katika jimbo kuu la Malindi kwamba watachukuliwa hatua za kinidhamu iwapo watakosa kuzingatia agizo hilo la Kanisa.

Wakati huo huo amesema Kanisa halikatazi mtu kushiriki ibada Kanisani bali halitakubali baadhi ya watu wenye ushawishi pamoja na wanasiasa kutumia vibaya sehemu za Ibada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version