News
Askofu Lagho: Marufuku Siasa Kanisani

Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo mkuu la Malindi Willybard Lagho, ametoa onyo kali kwa viongozi wa kisiasa dhidi ya kutumia vibaya Kanisa na kuendeleza maswala ya kisiasa na utakatishaji fedha.
Askofu Lagho amesema Kanisa hilo halitakubali viongozi wa kisiasa kulitumia vibaya kwa manufaa yao binafsi, akisisitiza haja ya wanasiasa kuheshimu sehemu za Ibada.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Askofu Lagho amesema mwanasiasa yeyote atakayemujulisha kiongozi wa kanisa kuhusu mipango yake na ibada maalum atakazoshiriki Kanisani hafai kutambulishwa Kanisani.
Askofu Lagho amewaonya mapadre na viongozi wa makanisa katoliki katika jimbo kuu la Malindi kwamba watachukuliwa hatua za kinidhamu iwapo watakosa kuzingatia agizo hilo la Kanisa.
Wakati huo huo amesema Kanisa halikatazi mtu kushiriki ibada Kanisani bali halitakubali baadhi ya watu wenye ushawishi pamoja na wanasiasa kutumia vibaya sehemu za Ibada.
News
Mbogo: Kaunti ya Mombasa Imeshindwa Kutatua Mzozo wa Ardhi

Aliyekuwa mbunge wa Kisauni Ali Mbogo ameikosoa serikali ya kaunti ya Mombasa kwa kushindwa kutatua suala tata la uskwota linalowakumba wakaazi wengi wa kaunti hiyo.
Akizungumza katika eneo la Kisauni katika kaunti ya Mombasa, Mbogo amesema tatizo la uskwota limeendelea kuwa chanzo kikuu cha migogoro ya ardhi na ukosefu wa usalama katika maeneo mengi ya kaunti ya Mombasa huku serikali ya kaunti hiyo ikionekana kulifumbia macho suala hilo.
Mbogo amedai kwamba maelfu ya wakaazi wa Kisauni na Mombasa kwa jumla wanaishi kwa hofu ya kufurushwa katika ardhi zao walizoishi tangu jadi kufuatia ukosefu wa hati miliki.
Wakati huo huo amedokeza kwamba baadhi ya maafisa wa serikali ya kaunti hiyo wanahusishwa na visa vya uporaji wa ardhi za umma kwa kushirikiana na waekezaji jambo ambalo amelitaja kuwa dhulma.
News
Tuko Tayari Kufuzu Kombe La Dunia

Nahodha wa Kikosi cha Soka vijana chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 Rising Stars Amos Wanjala amesema kwamba lengo lao kuu ni kufuzu kombe la dunia kwenye fainali ya mashindano ya Afcon kwa chipukizi iliofungua milango yake weikndi hii mjini Cairo Misri.
Akizungumza akiwa kambini mjini Cairo Wanjala anamini kwamba wana kikosi bora cha kuandikisha matokeo chanya kwenye kombe hilo licha ya kuwa ni mara yao ya kwanza kushiriki katika kipute hicho.
“Tuko tayari kufuzu World cup maana tumekua tukijiandaa vyema kwa mashindano haya,nataka niwatoe hofu wakenya kwamba kundi letu ni la kifo kwani wawe tayari kupata burudani kutoka kwetu.”
kwa Mujibu wa tineja huyo wa academia ya Nasty Sports ya Uhispania ni kwamba licha mabadiliko ya hali ya anga akilinganisha na Kenya kila mmoja yuko tayari kuonyesha uwezo wake katika jukwaa hili.
“Tuko syched up kucheza na mpinzani yeyote,kila mmoja amejiandaa vizuri kutendea haki na kupeperusha bendera ya taifa letu. Nikitaka kushukuru wizara ya michezo pamoja na shirikisho kwa kutuunga mkono kuanzia mwanzo wa mazoezi yetu mpaka mandhari ambayo tumepata hapa.”
Vijana wa nyumbani wanafungua kampeni dhidi ya Morocco May 1 wakiwa kundi B pamoja na Tunisia na vilevile Nigeria