Sports

George Foreman: Bingwa wa Masumbwi Afariki Dunia Akiwa na Miaka 76

Published

on

Bingwa wa zamani wa masumbwi kwa uzito wa juu George Foreman, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia yake na kunukuliwa na vyombo vya habari, Foreman alifariki huko nchini Marekani.
Foreman alijulikana sana Kwa kuzipiga ngumu na pambano lake la kihistoria, likiwemo lile la Rumble in the Jungle mwaka 1974 dhidi ya Muhammad Ali jijini Kinshasa DRC ambapo alipigwa kwa KO.
Aliiweka rekodi kwa kuwa bingwa wa uzani wa juu mwenye umri mkubwa zaidi (miaka 45) aliposhinda taji hilo mwaka 1994.
Mbali na masumbwi, Foreman alipata mafanikio makubwa kibiashara, hasa kupitia majiko yake ya umeme ya kuchoma nyama George Foreman Grill, ambapo alifanikiwa kuuza zaidi ya majiko milioni 100 duniani kote.
Foreman ameacha familia kubwa, wakiwemo watoto wake 12, wanawake 7 na wanaume 5 na wote wanaitwa George.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version