National News
Viongozi wa ODM Wakashifu Wanaosherehekea Kuanguka Kwa Raila AUC
Viongozi wa Chama cha ODM wamewakashfu baadhi ya wakenya wanaosherehekea kushindwa kwa aliyekuwa mgombea wa Kenya katika wadhfa wa uwenyekiti wa Tume ya umoja wa Afrika AUC Raila Odinga wiki iliyopita.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho nchini, Gladys Wanga, ambaye pia ni Gavana wa kaunti ya Homabay wamesema japo hawakutarajia kwamba Odinga angeshindwa katika kinyang’anyiro hicho lakini walikubali matokeo.
Wakizungumza eneo bunge la Likoni katika kaunti ya Mombasa wakati wa kongamano la wajumbe wa chama cha ODM, Wanga amempongeza Rais William Ruto kwa kusimama na Odinga katika uchaguzi huo, akiwakosoa wale waliosherehekea kushindwa kwa Odinga na kuwataja kama wakenya wasio na uzalendo.
Kauli yake imeungwa mkono na Naibu Kinara wa Chama hicho nchini Abdulswamad Sharrif Nassir ambaye pia ni Gavana wa kaunti ya Mombasa akiwakosoa wale wanaodai kwamba serikali ya Kenya Kwanza ilimsaliti Odinga.