Zawadi: Ni wakati ubunge wa Ganze kuongozwa na Mwanamke

Zawadi: Ni wakati ubunge wa Ganze kuongozwa na Mwanamke

Mwanasiasa Zawadi Kingi amekosoa uongozi duni unaondelea kushuhudiwa katika eneo bunge la Ganze, akisema viongozi walio mamlakani wameonyesha wazi kushindwa kutimiza malengo ya wananchi.

Akizungumza katika eneo bunge la Ganze, Zawadi amesema wakati umefika sasa kwa wakaazi wa Ganze kufungua macho na kutathmini uongozi wa mwanamke, akisema viongozi waliokuwa wakichaguliwa wameshindwa kufanikisha maendeleo mashinani.

Zawadi ambaye alitangaza nia yake ya kuwania kiti cha ubunge wa Ganze wakati wa uchaguzi mkuu ujao mwaka wa 2027, ameahidi kulitatua suala la elimu, afya, sawa na kuendeleza miradi mingine muhimu, akisisitiza kwamba eneo bunge la Ganze linahitaji kiongozi Mwanamke.

“Wamekuwa kwa uongozi lakini hakuna walichofanyia wananchi wa Ganze, Ndovu wamekuwa wakiharibu mimea ya watu na hakuna suluhu lililotolewa, hospitali hazina madawa, maji ni changamoto na tena tuko na viongozi. Nawaomba munichague ili tubadilishe uongozi huu mabaya, wakati huo mwanamke anaweza”, alisema Zawadi

Zawadi alisema wakaazi wa Ganze wana jukumu la kutafakari na mapema kuhusu hatma yao ya maendeleo na kufanya maamuzi bora wakati wa uchaguzi, akiwarai wakaazi wa Ganze kutokubali kushawishiwa kisiasa.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi