Ziara ya Rais Ruto Pwani yasheheni ahadi nono

Ziara ya Rais Ruto Pwani yasheheni ahadi nono

Zaira ya rais William Ruto ya siku tano katika ukanda wa Pwani imeonekana kuwa na ahadi nono kwa wenyeji huku zaidi ya takribani shilingi bilioni 85 zikitengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo

Rais Ruto akiwa katika kaunti ya Mombasa, aliahidi utoaji wa hatimiliki za ardhi laki mbili kwa wenyeji, akisema suala hilo litatekelezwa baada ya mazungumzo na baadhi ya wamiliki wa ardhi wasiokupo.

Wakati wa halfa hiyo ya Mombasa, rais Ruto aliwakabidhi wakaazi wa Pwani zaidi ya hatimiliki za ardhi elfu 33 na kuahidi ugavi wa hatimiliki zengine za ardhi laki mbili.

Suala la mpango wa uchumi sawamati, rais aliahidi kima cha shilingi bilioni 10 huku shilingi bilioni 50 zikielekezwa kwa mradi wa dongo kundu.

Ujenzi wa gorofa ya 16 ya nyumba za bei nafuu kaunti ya Mombasa

Katika kaunti ya Kilifi, ziara ya rais haikuwa tu ziara ya uzinduzi wa miradi ya maendeleo bali pia ilisheheni ahadi ya shilingi bilioni 18.

Ambapo fedha hizo zimetengewa miradi mbalimbali ikiwemo shilingi bilioni 7 za ujenzi wa barabara hasa barabara ya kilimita 35 kutoka Tezo-Kakanjuni-Jaribuni hadi Ganze kwa shilingi bilioni 2.2, shilingi bilioni 12 zikitengewa usambazaji wa umeme huku shilingi bilioni 22 kufanikisha ujenzi wa nyumba za bei nafuu.

Mradi wa ujenzi wa nyuma za wafanunzi kwenye vyuo vikuu, vyuo vya kiufundi, na KMTC ukitengewa shilingi bilioni 2 huku ahadi ya hatimiliki elfu 200 ikiendelea kutolewa na rais kwa wenyeji.

Ziara ya rais Ruto katika kaunti ya Kwale ilisheheni pia ahadi ya mabilioni ya pesa, ujenzi wa nyumba za bei nafuu wa shilingi bilioni 15, shilingi bilioni 2 kwa mradi wa ujenzi wa bandari ya Shimoni, huku shilingi bilioni 1.8 kwa usambazaji wa umme miongoni mwa miradi mingine.

Mikakati ya usambazaji umme kwa umma wazinduliwa rasmi na Rais Ruto

Kaunti ya Lamu na Tanariver pia hazikiachwa nyuma katika ziara ya rais ambapo bandari ya Lamu ikimulikwa kwa upanuzi zaidi ili kufungua ajira kwa vijana sawa na ujenzi wa masoko huku soko la Mpeketoni ikitengewa shilingi milioni 290 huku shilingi milioni 315 kufanikisha ujenzi wa Ua kwenye hifadhi ya Tsavo sawa na kufutilia mbali uhifadhi ya Shirango katika wadi ya Bamba ili kuzuia mizozo ya wanyamapori.