Serikali imeongeza juhudi za kuimarisha uaminifu, utawala bora na maendeleo ya kidijitali nchini, ikilenga kuhakikisha matumizi salama ya mtandao, yakuaminika na yanayowanufaisha wananchi wote.
Akizungumza jijini Mombasa wakati wa ufunguzi wa kongamano la chama cha ukaguzi na udhibiti wa mifumo ya habari, Waziri wa Habari na Uchumi wa Kidijitali William Kabogo alisema kuwa mabadiliko ya kidijitali nchini yameendelea kushika kasi kwa kiwango kikubwa.
Kabogo alisisitiza kuwa serikali imejizatiti kuweka mifumo madhubuti ya kulinda data na taarifa za watumiaji, huku pia ikihamasisha uwajibikaji katika matumizi ya teknolojia.
Kabogo aliongeza kuwa usalama wa mtandao ni nguzo muhimu katika kukuza uchumi wa kidijitali na kuvutia uwekezaji.
Taarifa ya mwanahabari wetu
