Zaidi ya wajumbe 50 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni walikongamana jijini Mombasa kuangazia masuala mbalimbali ikiwemo uchumi samawati, Uvumbuzi na jinsi ya kulinda mazingira ya bahari katika bahari hindi ya magharibi ya Pwani.
Kongamano hilo la 13 la Sayansi ya habari katika bahari hindi ya Pwani ya Magharibi lililoandaliwa na Shirika la GIZ lililenga kuibuka na suluhu la kudhibiti kabini chafu ya bahari.
Robin Farrington ni Mshirikishi wa ustawishaji wa Shirika la GIZ ambaye alisema kupitia Sayansi na uvumbuzi wa bahari hindi umechangia pakubwa katika kulinda mazingira ya bahari, akisistiza haja ya wadua mbalimbali kushirikiana.
“Kile tuliona mapema ni sehemu ya uchumi samawati hasa ikiwa tunaweza kufanya kwa ushirikishi wa uchumi samawati endelevu inahitaji watu wote hasa jamii ya Pwani lakini pia mazingira bora ya asili endelevu. Kuna mashirika yanafanya kazi kwa usiri, hayaji pamoja, hayatoa habari, hayashirikiana katika teknolojia.”, alisema Farrington.
Katibu katika Idara ya Sayansi, utafiti na uvumbuzi nchini Prof Shaukat Abdulrazak alisema serikali imewekeza zaidi katika kuangazia sera zinazochangia usimamizi bora wa raslimali za bahari, akisema bandari ya Mombasa sio tu raslimali ya kanda ya Pwani bali hutagemewa na mataifa mengi ikiwemo afrika mashariki
“Bandari ya Kenya inasalia kuwa kitovu cha uchumi wetu wa kitaifa na najua vizuri kwa sababu naongoza kikao cha Lapset, ni mchezo wa mabadiliko, kwa hivyo bandari ya Mombasa sio tu raslimali ya kitaifa, ni mlango ya kanda ya afrika mashariki ikiunganisha mataifa yasio na bahari hasa, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, DRC hadi soko la kimataifa”, aliweka wazi Prof Shaukat.

Zaidi ya wajumbe 50 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni walikongamana jijini Mombasa kwa Kongamano la 13 la Sayansi ya habari katika Magharibi ya Pwani lililoandaliwa na Shirika la GIZ.
Shaukat hata hivyo aliwarai wadau mbalimbali ikiwemo watafiti kuja pamoja na kufanya Utafiti wa kina utakaosaidia kuibuka na data maalum ili kuchangia udhibiti wa uharibufu wa uchumi wa bahari na kulinda mazingira ya bahari na kuchangia usambazaji wa data za uvumbuzi na teknolojia.
Balozi Nancy Karigithu ambaye ni Mshauri wa masuala ya uchumi wa bahari katika Ofisi ya rais, alisema kua haja ya serikali, wasimamizi wa bandari na wale wa miji mkuu kushirikiana ili kurahisisha shughuli za bandari pamoja nakudhibiti msongamano wa upakuaji wa makasha bandarini.
“Nimetaja kuhusu uchafuzi wa bandari, namaanisha wakati viwanda vinatafuta kawi ya kijani, ni ngapi zinakuja na uwezo, na vipi tunawezapata kutoka kwa hamasa na kujenga uwezo wa wasimamizi wa miji pamoja na kuibuka na suluhu kwa bandari.”, alisema Balozi Nancy.
Naibu Chansela wa Chuo kikuu cha Pwani Prof James H.P. Kahindi alisema kutokana na ukuaji wa Teknolojia katika sekta ya uchumi samawati idadi kubwa ya wanafunzi kwenye vyuo vikuu wamechangia kubwa katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga ikiwemo kutoka kaunti ya Kilifi, akisema wataendelea kuwashirikisha wanafunzi katika kuendeleza uvumbuzi na utafiti bora ili kulinda mazingira.
Hata hivyo Issak Elmi ambaye ni mkuu wa kitengo cha ikolojia katika Mamlaka ya mazingira nchini NEMA alisema ni lazima serikali itanue juhudi zake za kulinda mazingira ya bahari ili kuhakikisha ustawi wa sekta ya uchumi samawati.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi
