News
Nuno: Usalama umeimarishwa msimu wa Pasaka
Kamanda wa Polisi kanda ya Pwani Ali Nuno amesema usalama umeimarishwa msimu huu wa sherehe za Sikukuu ya Pasaka huku akiwataka wakaazi pamoja na wageni wa wanaolenga kuzuru kanda ya Pwani kutokuwa na hofu.
Nuno amewahimiza abiria wa magari ya uchunguzi wa umma kuhakikisha madereva wanazingatia sheria za barabarani ili kudhibiti ajali za mara kwa mara.
Aidha amesema ajali nyingi ambazo zimekuwa zikifanyika zimekuwa zikisababishwa na madereva wasiokuwa waangalifu barabarani huku wengine wakiwa walevi, wachovu miongoni mwa tabia zingine zisizofaa.
Vilevile, ameyaonya magenge ya kihalifu katika kaunti za Kwale na Mombasa ambayo yamekuwa yakiwahangaisha wenyeji kwamba yatakabiliwa kisheria.