News

Mwadime: Visa vya Wakenya Kuteswa Nchini Saudia Vimepungua

Published

on

Katibu katika Wizara ya Leba nchini Shadrack Mwadime amesema visa vya wakenya kuteswa na kuuwawa katika mataifa ya ughaibuni hasa nchini Saudia Arabia vimepungua pakubwa.

Mwadime amesema kupungua kwa visa hivyo kumetokana na serikali kuchukua hatua hitajika za kutia saini mkataba wa makubaliano ya kazi baina ya nchi hizi mbili.

Mwadime amesema serikali ya Kenya inaendeleza mazungumzo na serikali ya Saudia ili kufanikisha mkataba huo na kuwawezesha wananchi kuwa huru pindi wanapopata ajira katika taifa hilo.

Katibu huyo amesema shughuli hiyo itakapofanikishwa ni wazi kwamba visa vya wakenya kuuwawa na kuteswa nchini Saudia vitasitishwa kabisa.

Wakati huo huo amewashauri wakenya kutembelea ubalozi wa Kenya ili kufahamisha ubalozi huo kuhusu kazi wanazoenda kuzifanya na kushauriwa zaidi kuhusu mwongozo wa jinsi watakavyoripoti visa vya unyanyasaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version