News

Gavana Mung’aro Ampiga Kalamu Katibu wake Martin Mwaro

Published

on

Gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Mung’aro amemuachisha kazi Katibu wa kaunti hiyo Martin Mwaro kutokana na utendakazi duni na ukosefu wa uadilifu.

Gavana Mung’aro amemteua Catherine Kenga ambaye ni Waziri wa Uchukuzi katika kaunti ya Kilifi kushikilia wadhfa huo kama Kaimu Katibu kwa miezi 6 wakati mchakato wa kujaza nafasi hiyo ukiendelea.

Katika kikao na Wanahabari mjini Kilifi, Msemaji wa Serikali ya kaunti ya Kilifi Mativo Johnathan amesema hatua hiyo imechukuliwa ili kuhakikisha wakaazi wa kaunti ya Kilifi wanapokea huduma bora na kwa usawa bila ubaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version