National News

Waliotuma Maombi ya Kujaza Nafasi ya Mwenyekiti wa Tume Hiyo ya Uchaguzi Kupigwa Msasa

Published

on

Jopo la uteuzi wa Makamishna wapya wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC, linatarajiwa kuanza zoezi la kuwapigwa msasa wakenya waliotuma maombi ya kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Tume hiyo ya uchaguzi.

Jopo hilo ambalo linaongozwa na Mwenyekiti wake Dkt Nelson Makanda liko na mda wa hadi tarehe 25 mwezi Aprili mwaka huu kuwa limepata Mwenyekiti wa IEBC pamoja na makamishna wapya.

Jopo hilo limewarai wakenya kuondoa hofu kwani baada ya zoezi hilo kukamilika, taifa litakuwa na makamishna wapya wa IEBC walio waadilifu na wenye kujitolea kufanikisha uchaguzi huru na haki.

Tayari majina ya wakenya 37, yameorodheshwa kati ya wale wanaomezea mate nafasi ya Mweyekiti wa IEBC ambao wanatarajiwa kuhojiwa ili kueleza wakenya malengo, dhamira na mikakati wataofanya kufanyika uchaguzi wa haki iwapo mtu atateuliwa kushinikilia nafasi hiyo.

Hata hivyo aliyekuwa msajili wa idara ya Mahakama nchini Ann Amadi, aliyekuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika mashariki Charles Nyachae, aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya Kenya Power Joy Brenda Masinde pamoja na aliyekuwa Afisa mkuu mtendaji wa IEBC James Oswago ni kati ya wakenya wanaomezea mate nafasi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version